pmbet

Mwandishi Al Jazeera alishikilia mateka 3 wa Israel nyumbani kwake

Eric Buyanza

June 10, 2024
Share :

Mwandishi wa habari wa Gaza ambaye alikuwa akifanya kazi na kituo cha Al Jazeera, alikuwa akiwashikilia mateka watatu wa Israeli kwenye nyumba anayoishi na familia yake kabla ya kuuawa na makomando wa Israel wakati wa operesheni ya uokoaji Jumamosi, Juni 8, kwa mujibu taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel. 

Abdallah Aljamal, ambaye pia alifanya kazi kama msemaji wa wizara ya kazi inayoendeshwa na Hamas, aliuawa wakati wanajeshi wa kikosi maalum walipovamia nyumba yake katikati mwa Gaza na kuwaokoa mateka Almog Meir Jan, Andri Kozlov, na Shlomi Ziv. 

Kifo cha Aljamal awali kiliripotiwa na Rami Abdu, mkuu wa (Euro-Med Human Rights Monitor), ambaye alidai wanajeshi wa Israel walivamia nyumba ya mwandishi huyo na kumuua yeye pamoja na watu kadhaa wa familia yake.

Jeshi la Israel (IDF) likasema Aljamal alikuwa akiwashikilia mateka ndani ya nyumba ya familia yake, lakini haikutaja kilichotokea kwa jamaa zake.

"Huu ni uthibitisho zaidi kwamba kundi la kigaidi la Hamas linatumia raia kama ngao," IDF ilisema katika taarifa yake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet