pmbet

Mwandishi mkongwe wa Uganda auawa kwa kupigwa risasi

Eric Buyanza

April 20, 2026
Share :

Mwandishi wa habari mkongwe nchini Uganda ameuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa karibu na nyumba yake huko Kawanda, wilaya ya Wakiso katika mji mkuu Kampala. Hayo yameelezwa Jumapili na Polisi.
 

Joe Nam, mwenye umri wa miaka 55, alifanya kazi katika vyombo vya habari vya serikali kwa miongo mitatu kabla ya kustaafu na aliandika kitabu kinachozungumzia matokeo yanayoweza kushuhudiwa Uganda pale Rais Yoweri Museveni aliyetawala nchi hiyo kwa muda mrefu atakapoondoka madarakani.
 

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Joe alipigwa risasi na kuuawa na mtu aliyejificha uso saa 7 usiku karibu na makazi yake huko Kawanda, katika wilaya ya Wakiso, ambapo mshambuliaji, baada ya kumpiga risasi alikimbia," ameeleza Naibu Msemaji wa Polisi Luke Owoyesigyire.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet