pmbet

Mwandishi wa habari afariki Mwanza

Sisti Herman

December 27, 2023
Share :

Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Blandina Aristides amefariki dunia jana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amesema, leo Jumanne Desemba 26, 2023 kuwa Blandina alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua na alijifungua kwa upasuaji, lakini hali yake ilibadilika ghafla na kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) mpaka umauti unamfika.

"Amefariki dunia leo asubuhi pamoja na mtoto wake," amesema Soko na kuongeza kuwa taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika Mabatini laini ya Polisi jijini Mwanza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet