pmbet

Mwandishi wa habari apigwa risasi akiwa kwenye majukumu yake.

Joyce Shedrack

July 17, 2024
Share :

Mwandishi wa habari wa Catherine Wanjeri Kariuki anayefanya kazi kwenye kampuni ya  Mediamax Limited, amepigwa risasi na polisi wakati akiwa kwenye majukumu yake katika mji wa Nakuru nchini Kenya akiripoti maandamano yaliyoongozwa na vijana maarufu kama Genz siku ya jana walipokuwa kwenye maandamano ya kushinikiza Rais William Ruto ajiuzulu.

 

Mwandishi huyo wahabari ambaye alikuwa amevalia sare rasmi za wanahabari na alikuwa amesimama pembezoni mwa barabara  alipigwa risasi iliyomlenga kwenye paja la mguu wake wakati maafisa wa kiusalama wakikabiliana na waandamanaji na baada ya kupigwa risasi kundi la vijana wa Genz lilijitokeza kumsaidia na kumkimbiza katika Hospitali ya Valley.

 

Baraza la Wanahabari Kenya MCK na Baraza la Mawakili Kenya LSK wamepinga vikali suala la maafisa wa usalama wa Nchi hiyo kutumia nguvu wakati wa kukabiliana na waandamanaji huku wakitumia silaha na kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia.

MediaMax ni kampuni inayomiliki vyombo vya habari zaidi ya kimoja Nchini humo ikiwemo K24 TV ,Milele FM pamoja na kituo cha redio na Runinga cha lugha ya Kikuyu, Kameme FM na Kameme TV.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet