Mwandishi wa Marekani jela miaka 16, akituhumiwa kufanya ujasusi nchini Urusi
Eric Buyanza
July 20, 2024
Share :
Mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich jana Ijumaa Julai 19 alihukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa kosa la kufanya ujasusi nchini Urusi, ingawa shutuma hizo zimekataliwa mara kwa mara na mtuhumiwa.
Mwandishi huyo alikamatwa mwishoni mwa mwezi Machi 2023, alipokuwa akifanya kazi yake ya uandishi wa habari huko Yekaterinburg katika jimbo la Urals, na akatuhumiwa kufanya Ujasusi.