Mwanzo mbaya kwa Pochettino, ila kuna mwanga mbele
Sisti Herman
November 22, 2026
Share :

Mwanzo mbaya kwa Pochettino, lakini at least ataondoka na Positives nyingi za kuanza kuboresha, IMENYESHA NA AMEONA PANAPOVUJA
Hii ni tathmini yangu ya mchezo;
1. Squad Selection
Dakika 10 za mwanzo alivyoingia na 4-2-3-1 yenye mabeki watatu asilia wa kati nilielewa kuwa itakuwa 3-2-4-1(asymmetric 4-2-3-1) ambapo Dalot atakuwa anasogea zaidi juu usawa wa Bruno, Cunha na Dorgu kisha De Ligt, Yoro na Martinez wakibaki nyuma ya Youri na Mainoo
Kilichomuangusha hapa ni namna hiyo Back 3 inavyogawana majukumu, DE LIGT was a BAD MOVE ya SELECTION YAKE, na huyu ndiye aliyemsababishia Yoro Red Card, mechi iliishia hapo kimatokeo

2. Tactical Reaction to Red Card
Baada ya Red Card akamtoa Mbeumo na kumuingiza Maguire na System ikabadilika kutoka 4-4-1 after Red Card na kuwa 5-3-1 inayozuia zaidi chini (mid-low block), mwanzo nilidhani kuwa ilipaswa kubaki 4-4-1, lakini kwa namna walivyocheza baada ya Sub nilikumbuka kuwa 5-3-1 ni bora kuliko 4-4-1 kwasababu ile ni United, siyo timu nyingine
Wachezaji wa United hawakimbii so 4-4-1 ingezuia na depth kubwa kama ile United ya Carrick, lakini 5-3-1 ilizuia vizuri sana (compact shape, unity), that was 1st positive take leo

3. 2nd Half Tactical Subs
Kwenye Subs za 2nd half, nilidhani angetoka Dalot aingie Mazraoui badala ya kutoka Dorgu, at least kwenye Counter Attack Mazraoui na Dorgu wangeweza kuitoa timu vizuri kuliko Dalot
Pia baada ya Zirkzee kuingia nyakati nyingi United ilijikaba kwasababu ilihitaji kutoka kwa Counter Attacks lakini yeye ni mzuri zaidi ku-link play kuliko kushambulia space, kwahiyo kila akipewa mpira hakuona mtu wa kumpa mpira mbele ndiyo maana muda mwingi alilipa goli mgongo.
4. Poor Rest Defence
Moment ya bora kwa United baada ya magoli mawili ya mwanzo ilikuwa kuzuia vizuri bila mpira, LAKINI Moment dhaifu zaidi kwa United ilikuwa Reaction yao pale wanapopoteza mpira, hii haikuwa kwa wachezaji bali kwenye system, hawakuwa na Rest Defence nzuri kumeza mashambulizi ya kujibu ya Liverpool.
Rejea magoli mawili ya Liverpool ya mwisho, la Rio na la Munoz, yote yametokana na United kushindwa kukabiliana na hizo Defensive Transtions, nadhani ni kwasababu hawakujiandaa na kuwa wachache uwanjani kwasababu most of time walikutwa kwa idadi ndogo nyuma

5. Poor Rest Attacks
Kwasababu ya nyakati nyingi kucheza chini (mid-low block) Outlet pekee ya United kushambulia ikawa ni Counter Attacks, napo hizo Counter attacks ni kama hawakujiandaa nazo kwasababu hazikuwa na ubora, Walichelewa kutoka haraka na kwa idadi sahihi kuvizia kabla Liverpool hawajarejea kwenye muundo wao mzuri wa kuzuia
Dorgu/Mazraoui na Dalot walichelewa kuongeza idadi kwakushambulia space nyuma kina Kerkez na Frimpong kwa haraka, Bruno, Mainoo na Tielemans walichelewesha kuweka mali kwenye njia, pia Zirkzee hakuwa mzuri kushambulia space behind backline ya Liverpool hapo sasa Offensive Transitions zao zikawa dhaifu kuidhuru Liverpool






