Mwarabu ashinda kuwa Senetor Marekani
Sisti Herman
November 4, 2026
Share :

Mgombea wa Chama cha Democratic, Abdul El-Sayed, ameshinda uchaguzi wa Seneti ya Marekani katika jimbo la Michigan, akimshinda mpinzani wake wa Chama cha Republican, Mike Rogers.
Ushindi huo unamfanya El-Sayed kuwa Mwislamu wa kwanza kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Seneti ya Marekani, kwa mujibu wa taarifa za matokeo ya uchaguzi.
El-Sayed, ambaye ana asili ya Misri, alikuwa akiwania kiti hicho katika uchaguzi wa Novemba 3, 2026, akichuana na Rogers katika kinyang’anyiro kilichokuwa kikifuatiliwa kwa karibu kutokana na umuhimu wake katika kuamua chama kitakachodhibiti Seneti.
Ushindi wake ni hatua muhimu katika historia ya uwakilishi wa Waislamu katika siasa za Marekani, ambako hakuna Mwislamu aliyekuwa amewahi kuhudumu katika Seneti kabla ya uchaguzi huu.





