Mwarabu awaweka meza moja Ronaldo, AJ, Fury na Ngannou
Sisti Herman
March 7, 2024
Share :
Mshauri wa familia ya kifalme ya Saudia Turki Alalshikh amekutana mabondia wa daraja la juu zaidi duniani Tyson Fury, Francis Ngannou na Antony Joshua pamoja na mwanasoka bora maarufu zaidi Cristiano Ronaldo ambao wote kwa pamoja ni sehemu ya msimu wa Riyadh Season ambao hujumuisha tamasha linaoandaa michezo mbalimbali kama Masumbwi na mpira wa miguu.
“Nikiwa na marafiki zangu wapendwa, wanamichezo bora zaidi duniani katika michezo yao na hivi karibuni tuna mradi na gwiji Cristiano Ronaldo huko Riyadh utatangazwa katika miezi ijayo wakati tunasubiri pambano siku ya Ijumaa kati ya Joshua na Anganou... na tunatarajia pambano la karne kati ya mabingwa wasio na ubishi Tyson dhidi ya Usyk” aliandika kupitia mitandao yake ya kijamii msomi huyo ambaye familia ya kifalme ya Saudia humtumia kuandaa miradi mikubwa ya biashara inayohusisha burudani na michezo.
Kwa miaka ya hivi karibuni msimu wa Riyadh umeandaa matukio makubwa ya michezo ikiwemo kuimarisha ligi ya Saudia kwa kuwavuta wachezaji wakubwa kama Ronaldo, Neymar na wengine, kuandaa mapambano makubwa ya masumbwi na matamasha ikiwemo mechi iliyowakutanisha Messi na Ronaldo.