Mwendesha mashataka ataka wanachama 25 wa M23 kuhukumiwa kifo
Eric Buyanza
July 30, 2024
Share :
Mwendesha mashataka nchini Congo amependekeza hukumu ya kifo kwa washtakiwa 25 wanautuhumiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi la M23 katika kesi inayoendelea mjini Kinshasa.
DW imeripoti kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya uhalifu wa kivita, kushiriki katika uasi na uhaini.
Kundi la M23 linaoongozwa na watutsi na kuungwa mkono na Rwanda limeyateka maeneo makubwa ya ardhi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwishoni mwa 2021.