Mwenye rekodi ya kadi nyekundu alianza ukocha na kadi nyekundu.
Joyce Shedrack
April 20, 2026
Share :
Gerardo Alberto Bedoya Múnera ni mchezaji wa zamani wa soka wa Kolombia na kocha wa sasa. Alianza kucheza kama beki lakini pia alicheza kama kiungo mkabaji.

Nyota huyo alipewa jina la utani "The Beast" (Mnyama), kwa sasa anashikilia rekodi ya dunia ya kupata kadi nyekundu nyingi zaidi (46) katika historia ya mchezo wa soka.
Hata baada ya kuanza ukocha, aliendelea na rekodi hiyo kwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mechi yake ya kwanza tu akiwa kocha msaidizi wa klabu ya Independiente Santa Fe Machi 23, 2016.





