Mwezi mmoja baada ya kujifungua, akutwa na mtoto mwingine tumboni
Eric Buyanza
April 15, 2025
Share :
Huko nchini Afrika ya Kusini, mwanamke mmoja amekua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kugundulika ana mtoto mwingine tumboni ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kujifungua.
Taarifa zinasema baada ya mwanamke huyo kutimiza mwezi tangu ajifungue alianza kusikia hali isiyo ya kawaida kwenye mwili wake, jambo lililowalazimu watu wake wa karibu kumkimbiza hospitali.
Kilichowashtua wengi ni majibu ya vipimo kuonyesha kuwa mwanamke huyo alikuwa na mtoto mwingine tumboni, ambapo madaktari walimuandaa na akajifungua tena.
Kwasasa mwanamke huyo ana mapacha ambao wamepishana mwezi mmoja.