Mwezi wa damu' kushuhudiwa Afrika wikendi hii
Eric Buyanza
September 4, 2025
Share :
'Mwezi wa damu' utashuhudiwa angani wikendi hii, kutokana na kupatwa kamili kwa mwezi.
Watakaokuwa na fursa ya kutazama mwezi huo angani wataona mwezi wote ukibadilika kuwa rangi ya wekundu Septemba 7, 2025.
Kupatwa kwa mwezi kutaonekana katika sehemu za Afrika, Asia, Australia na Ulaya.
Tofauti na matukio mengine ya kupatwa kwa mwezi ambako mtazamaji huitaji miwani maalum na vifaa vingine ili kuweza kutazama angani, kupatwa huku kwa mwezi kunaweza kuonekana kwa urahisi: hakuhitaji muda maalum, vifaa, ujuzi au mpangilio.
Mtazamaji atatazama moja kwa moja kwenye Mwezi wakati tukio hilo linatokea.
Tukio hili adimu litaonekana kwa zaidi ya watu bilioni saba duniani kote, huku takriban bilioni 6.2 wakiweza kushuhudia tukio lote kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kupatwa kwa jua siku hiyo itakuwa ndio tukio refu zaidi la kupatwa kwa mwezi tangu 2022, likiwa na jumla ya saa 1 na dakika 22, ambapo Mwezi utakuwa na rangi nyekundu ya wekundu.
BBC