pmbet

Mwigizaji Carina aliyeugua kwa miaka 9 na kufanyiwa upasuaji mara 25 amefariki dunia.

Joyce Shedrack

April 15, 2025
Share :

Mwigizaji wa filamu Hawa Hussein maarufu Carina amefariki dunia leo Aprili 15,2025 akiwa nchini India alikoenda kupatiwa matibabu ya tumbo yaliyokuwa yanamsumbua kwa miaka mingi.

carina (2) – Global Publishers
Taarifa ya kifo cha msanii huyo zimethibitishwa na mwandishi mkongwe wa habari Imelda Mtema ambaye alikuwa mtu wake wa karibu aliyekuwa akisaidiana na familia yake kusimamia matibabu ya Carina.

"Ni kweli amefariki dunia nimepigiwa simu leo na watanzania waliopo India ambao walikuwa wanaishi naye na kumsaidia  jana tu nimeongea naye," amesema Imelda akiwa kwenye mahojiano na Global Tv.

Mwigizaji huyo alitarajiwa kurejea nchini leo baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa kutibu tatizo la tumbo lililokuwa likimsumbua kwa kipindi cha miaka tisa huku akifanyiwa upasuaji wa tumbo zaidi ya mara 23.

Hawa aliondoka nchini Februari 24, 2025 kwenda India kupatiwa matibabu baada ya kukamilika kwa taratibu za safari na gharama ya matibabu Sh54 milioni ambazo zilitokana na michango ya serikali na tasisi mbalimbali zilijitokeza kumchangia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet