Mwigizaji Johnny Wactor wa ' General Hospital' afariki dunia
Sisti Herman
May 27, 2024
Share :
Mwigizaji kutoka Marekani Johnny Wactor ambaye alijulikana zaidi kupitia tamthilia ya ‘General Hospital’ amefariki dunia kwa kupigwa risasi katika moja ya mtaa wa Los Angeles.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na mama yake mzazi Scarlett Wactor ambapo aliviambia vyombo vya habari siku ya jana Jumapili Mei, 26, 2024 kuwa mwanaye alipigwa risasi na wezi watatu waliotaka kuiba kwenye gari lake siku ya Jumamosi asubuhi.
Wactor amefariki akiwa na umri wa miaka 37, huku akionekana kwenye tamthilia kama ‘Lifetime’, ‘Hollywood Girl’, ‘The Passenger’ na nyinginezo.