Mwigizaji maarufu wa Marekani Erick Dane afariki Dunia.
Joyce Shedrack
February 21, 2026
Share :
Mwigizaji maarufu wa Marekani Eric Dane amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 53 baada ya kupambana na ugonjwa wa ALS (Amyotrophic Lateral Sclerosis) ambapo taarifa kutoka kwenye familia yake zimeeleza kuwa Eric alifariki akiwa nyumbani kwake. 
Eric Dane alijipatia umaarufu mkubwa duniani kupitia nafasi yake ya Dk. Mark Sloan maarufu kama “McSteamy” katika tamthilia ya hospitali ya Grey’s Anatomy, uigizaji ambao uliifanya nafasi hiyo kuwa miongoni mwa Wahusika waliopendwa zaidi katika historia ya tamthilia hiyo na kisha baadae alionekana pia katika tamthilia ya kijeshi ya The Last Ship, ambapo aliigiza kama Kamanda Tom Chandler.
Katika miaka ya karibuni, alirejea kwenye uigizaji kwa mafanikio makubwa kupitia tamthilia ya HBO Euphoria akiigiza kama Cal Jacobs nafasi ambayo ilimletea sifa mpya na kumtambulisha duniani.
Dane alishiriki pia katika filamu kadhaa za Hollywood zikiwemo X-Men: The Last Stand ambako aliigiza kama Multiple Man, pamoja na Valentine’s Day.





