Mwigulu atoa majiko ya gesi 900!
Eric Buyanza
January 12, 2024
Share :
Mbunge wa Iramba Magharibi, Dk. Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Fedha ametoa majiko ya gesi 900 kwa Mama lishe na Baba lishe kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mitungi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya hiyo kwa niaba ya Dk. Nchemba alisema mitungi hiyo imetolewa na mbunge huyo kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za utunzaji wa mazingira kazi ambayo aliianza tangu alipokuwa Makamu wa Rais.