Mwimbaji wa nyimbo za Injili Gogo Afariki Dunia.
Joyce Shedrack
September 4, 2025
Share :
Muimbaji wa nyimbo za Injili Kutoka Uganda Musabyimana Gloriose Maarufu kama "Gogo" amefariki Dunia taarifa za kifo chake zikitolewa na aliyekuwa manager wake Bruno K huku chanzo cha kifo chake bado hakijatajwa.
Gogo wimbo wake maarufu wa "Everyday, I Need Blood of Jesus," ulimpatia umaarufu zaidi watu wakivutiwa na sauti yake ya kitakatifu pamoja na ujumbe uliopo ndani ya nyimbo zake, GoGo ameacha Majonzi makubwa kwa Mashabiki zake ambao kwa hivi sasa wanaomboleza kwa ku-share Clip za Nyimbo zake alizokuwa akifanya kabla ya umauti kumkuta wakimuenzi kwa alama aliyoiacha Duniani kwa namna alivyotumia maisha yake kumtumikia Mungu.