pmbet

MWISHO WA DOLA AFRIKA? China yasambaza sarafu ya Yuan kimya kimya

Eric Buyanza

August 19, 2026
Share :

Serikali ya China imeweka mkakati thabiti wa kuimarisha ushawishi wa sarafu yake, Yuan (RMB), katika bara la Afrika ili kupunguza utegemezi wa dola ya Marekani.
 

Mkakati huu unalenga kubadilisha nguvu kubwa ya kibiashara ambayo China inayo barani Afrika kuwa ushawishi wa kifedha.

 

Benki kuu na za kibiashara barani Afrika zinaunganishwa na mfumo wa malipo wa China wa Cross-Border Interbank Payment System (CIPS).
 

Mfumo huu ni mbadala wa mfumo wa kimataifa wa SWIFT unaodhibitiwa zaidi na mataifa ya Magharibi.

 

Benki ya Standard Bank, ambayo ni kubwa zaidi Afrika, tayari inaruhusu malipo ya moja kwa moja ya Yuan katika nchi 19 za Afrika (ikiwemo kupitia Benki ya Stanbic nchini Tanzania).
 

Zambia mapema mwaka huu, ilianza kukusanya kodi na mirabaha (royalties) kutoka kwa makampuni ya madini ya China kwa kutumia sarafu ya Yuan.

 

Kwa upande wa Kenya, sehemu ya madeni ya ujenzi wa reli (SGR) yaliyotakiwa kulipwa kwa dola yamebadilishwa na sasa yanalipwa kwa Yuan.

 

Pia China imeingia mikataba na nchi kama Misri, Nigeria, na Afrika Kusini ili kuruhusu biashara kufanyika moja kwa moja kwa sarafu zao za ndani na Yuan bila kupitia dola.

 

Angola nao wameruhusu benki zake za kibiashara kutumia Yuan kama sehemu ya akiba ya kigeni ya lazima.


 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet