pmbet

Mwisho wa ubishi...! Klopp kumkaribisha Pep kwa mara ya mwisho

Sisti Herman

March 10, 2024
Share :

Ligi Kuu England inaendelea tena leo Machi 10, 2024 kwa mechi tatu katika viwanja tofauti huku kukiwa na mtanange ambao huenda ukaamua mwelekeo wa mbio za ubingwa.

Liverpool watakuwa wenyeji wa Mabingwa watetezi, Manchester City katika dimba la Anfield majira ya saa 12:45 jioni huku kila mmoja akihitaji ushindi ili kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.

Kila timu ina fursa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City ikitazamia kutetea ubingwa huo na kubeba kwa mara ya nne mfululizo huku Majogoo wakitazamia kufikia rekodi ya Manchester United ya makombe 20 ya Ligi.

Mchezo huo unawakutanisha kocha wa pili na wa tatu kuhudumu kwa muda mrefu kwenye EPL Jurgen Klopp na Pep Guardiola mtawalia. Wawili hao wanakutana kwa mara ya 30 leo.

Klopp na Pep tayari wamekutana mara 29 huku Mjerumani huyo akishinda mara 12 huku Guardiola akishinda mara 11 na sare sita.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet