pmbet

Mwizi wa kuku aambiwa achague moja, kumla mbichi au apigwe?

Eric Buyanza

January 20, 2024
Share :

Mwizi mmoja amelazimishwa kula kuku mbichi baada ya kunaswa kwenye banda la kuku akiiba huko Bulawayo nchini Zimbabwe.

Baada ya kunaswa eneo la tukio mwizi huyo wa kuku aliomba asamehewe kwani Januari tu imekuwa ngumu kwake kama ilivyo kwa watu wengine.

 

Hata hivyo maombi yake yaliangukia kwenye masikio ya wasio na huruma, baada ya kundi la watu kumtaka achague moja apewe kipigo au atafune kuku mmoja akiwa mbichi.

 

Bila kusita mwizi huyo alichagua kula kuku mbichi huku akishuhudiwa na umati wa watu na wengine wakirekodi tukio hilo kupitia simu zao za mkononi.

 

"Damu ikichuruzika kutoka kwenye kona ya midomo yake, mara kwa mara alikuwa akikohoa manyoya moja au mawili huku akikunja uso kama mtu anayemeza nyongo. Vipigo, kwa namna fulani, vilikuwa vibaya zaidi kwake kwani alikula chakula kisichompendeza ili kuwazuia watu wenye hasira wasimtandike. Nafikiri hatakula kuku tena katika maisha yake.” alisema shuhuda mmoja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet