Mzalishaji mkubwa zaidi wa kondom atangaza kupandisha bei
Eric Buyanza
April 23, 2026
Share :

Kampuni ya Carix ambayo ndiye mzalishaji mkubwa zaidi wa kondomu duniani imetangaza kuwa itaongeza bei ya bidhaa hizo kwa 30% au zaidi iwapo vita vitaendelea nchini Iran.
Kampuni hiyo iliopo nchini Malaysia, imesema vita vinavyoendelea Iran, vimefanya iwe vigumu kupata mali ghafi ya kutengeneza kondomu.
Goh Mia Kat, mkurugenzi wa Carex, alisema gharama ya kutengeneza kondomu hizo imepanda tangu vita kuanza.
Carex huzalisha zaidi ya kondomu billioni 5 kila mwaka na huuzia makapuni makubwa kama Durex na Trojan, ikiwemo na wizara za afya za serikali mbalimbali.
Goh alitoa taarifa hiyo katika mahojiano na shirika la habari la Reuters na Bloomberg.





