Mzamiru aongezwa miaka miwili Simba
Sisti Herman
June 25, 2024
Share :
Klabu ya Simba imemuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wa kati Mzamiru Yassin kuendelea kuwatumikia klabu hiyo mpaka 2026.
Mzamiru aliyejiunga na Simba Julai 2016 akitokea Mtibwa Sugar ameendelea kuwa na kiwango bora kiasi cha kuendelea na makocha mbalimbali waliopita msimbazi kwa nyakati tofauti.
Mzamiru akimaliza mkataba huo atakuwa ametimiza miaka 10 ya kuitumikia Simba.