Mzamiru Yassin apewa 'Thank You' baada ya miaka 10 ndani ya Simba.
Joyce Shedrack
July 17, 2026
Share :
Klabu ya Simba imehitimisha rasmi ushirikiano wake na kiungo mkabaji Mzamiru Yassin Said Selemba baada ya kuitumikia timu hiyo kwa takribani miaka 10 tangu alipojiunga mwaka 2016 akitokea Mtibwa Sugar.

Katika kipindi chake akiwa Msimbazi, Mzamiru alijijengea heshima kubwa kutokana na kujituma, nidhamu na uwezo wake wa kulinda safu ya kiungo.
Miongoni mwa mafanikio aliyoyapata akiwa Simba ni kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mataji matatu ya Kombe la Shirikisho (FA Cup), mataji matano ya Ngao ya Jamii, pamoja na Kombe la Mapinduzi.
Aidha, alikuwa sehemu ya kikosi kilichofika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2021 na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2022, mafanikio yaliyoiweka Simba katika ramani ya soka la Afrika.





