pmbet

Mzee Magori atuliza upepo mbaya Simba, awaasa watulie

Sisti Herman

April 11, 2024
Share :

Baada ya kuandamwa na matokeo mabaya hali iliyoamsha hisia kali za mashabiki wa Simba, aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Crestus Magori ameandika waraka mzito kuhusiana na hali ilivyo ndani ya klabu hiyo na kumtaja pia Mwekezaji na Rais wa heshima Mohamed Dewji.

Anaandika Mzee Magori
_____

Wana-Simba naomba tutulie! Hakuna safari isiyokuwa na mabonde wala miinuko!

Safari ya Simba mpya ilianza mwaka 2018, safari ambayo mpaka sasa haijakamilika! Mategemeo ya kila Mwana-Simba ni kuwa baada ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka huu (2024) January, Serikali itakamilisha mchakato huo hivi karibuni!

Katika kipindi hiki cha miaka 6 ya Simba mpya, Timu imepiga hatua kubwa kimaendeleo kama ifuatavyo;

1. Kutoka katika Timu isiyojulikana ni ya ngapi Afrika (unranked) mpaka namba 5 Afrika
2. Kutoka bajeti ya Tshs 3bn mpaka bajeti ya zaidi ya Tshs 20bn
3. ⁠Timu imechukua Ubingwa wa Tanzania mara 4
4. ⁠Ubingwa wa FA mara 3
5. ⁠Ngao ya jamii mara 4
6. ⁠Robo fainali ya Champions league mara 4
7. ⁠Robo fainali ya Confederation Cup mara 1
8. ⁠Ushiriki wa African Football league katika Timu 8 bora Afrika
9. ⁠Viwanja vyake vya mazoezi
10. ⁠Team ya Wanawake Simba Queens kuchukua Ubingwa mara 3
11. ⁠Team ya Wanawake Simba Queena kufika Nusu Fainali ya Champions League ya wanawake Africa

Mafanikio haya katika kipindi cha miaka 6 siyo madogo kwa namna yoyote ile! Hakuna Timu yoyote Tanzania iliyowahi kufikia mafanikio haya!

Hongera Mo Dewji, Bodi ya Simba na Menejimenti ya Klabu, Walimu, Wachezaji na kila Mwana-Simba!

Nafahamu hamu ya Wanasimba ni kurudisha Ufalme wetu hapa nyumbani na kuvuka hatua ya robo fainali kwenye michuano ya CAF!

Ndoto hizi haziwezi kufikiwa kwa mabishano, mvurugano na ugomvi bali kwa kukaa chini na kujipanga kimkakati!

Naomba niwahakikishie baada ya mazungumzo na Raisi wa Heshima wa Klabu Mohamed Dewji naomba niwatoe hofu kuwa Mo hajawahi kuiacha Simba na hataiacha Simba na kuanzia sasa atashirikiana na Uongozi kujipanga upya kurudisha heshima ya Simba na kuzidi kuimarika!

Tuachane na kelele za mitandaoni, tuwe nyuma ya Timu yetu! Simba imara inakuja!

Simba nguvu moja!

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet