Mzee Rashid aliongeza mke wa 7 akiwa na miaka 110, amekufa na miaka 142
Eric Buyanza
March 26, 2026
Share :
#JeWajua Nasser bin Radan Al Rashid Al Wadaei, mtu aliyeaminika kuwa mzee zaidi nchini Saudia Arabia alifariki mwezi January 2026 akiwa na umri wa miaka 142, na kuacha watoto 134 na wajukuu wa kutosha.
Inaelezwa kuwa alipofikisha umri wa miaka 110 Mzee Rashid alioa mke wa saba ili aendelee kupanua familia yake.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Saudia, Mzee huyu alikuwa mtu anayeheshimika sana katika jamii, anayejulikana kwa kuheshimu imani yake.
Nasser bin Radan alifariki Januari 8 mwaka huuu huko mjini Riyadh na kuzikwa katika nyumba ya baba yake, zaidi ya watu 7,000 walihudhuria mazishi yake kwenye mji wa Dhahran.






