Mzee wa miaka 65, mbaroni kwa kubaka kitoto cha miaka 7
Eric Buyanza
June 28, 2024
Share :
Mzee wa miaka 65, aliyefahamikwa kwa jina la Francis Ogwu, anashikiiwa na polisi nchini Nigeria akidaiwa kumbaka binti wa miaka 7.
Mzee huyo anatuhumiwa kumbaka mtoto huyo mara tatu, na alikuwa akimpatia pesa (naira 1000, sawa na shilingi 1,700 za kibongo) kila baada ya kumfanyia kitendo hicho.
Taarifa ya tukio hilo ilifikishwa Ustawi wa Jamii na baada ya kubanwa kisawasawa mzee huyo ....alijitetea kwa kusema alishawishika kufanya kitendo hicho kwa sababu mke wake huwa anatoa visingizio vingi kila wakati anapomuhitaji kinyumba.
Hata hivyo maafisa wa ustawi wa jamii walilifikisha swala hilo polisi ambao walimchukua na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.