Mzize hakamatiki ufungaji Shirikisho
Sisti Herman
May 16, 2024
Share :
Wakati wikiendi hii zikitarajia kuchezwa mechi za nusu fainali ya kombe la shirikisho (CRDB Federation Cup) mshambuliaji Kinda kinda wa klabu Yanga Clement Mzize anaongoza kwa utupiaji wa mabao akiwa na magoli matano.
Hii ni orodha ya wachezaji watano bora kwa ufungaji;
1. Clement Mzize, Yanga - 5
2. Edward Songo, JKT - 5
3. Yohana Mkomola, Tabora - 4
4. Joseph Guede, Yanga - 3
5. Sadio Kanoute, Simba - 3
Nusu fainali ya michuano hiyo ityaendelea wikiendi hii kwenye majiji mawili tofauti;
- Mwanza; Mei 18, Azam vs Coastal Union
- Arusha, Mei 19, Yanga vs Ihefu
Fainali ya michuano hiyo msimu huu itachezwa kwenye dim,ba la Tanzanite Kwaraa mjini Babati, Manyara.