Mzizima derby yavunja fungate la Yahya Zayd.
Joyce Shedrack
September 15, 2026
Share :
Mchezo wa Mzizima Derby unaozikutanisha timu za Azam FC na Simba umevunja Fungate la kiungo wa Azam FC, Yahya Zayd aliyefunga Ndoa Jumapili, Jijini Dar es Salaam.

Yahya amefunga Ndoa na Mtangazaji wa Kituo cha Habari (Azam TV) Fatuma Chikawe na jana jioni Yahya alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji wa timu hiyo waliofanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo.
Pambano hilo la Ligi Kuu Bara linatarajiwa kuchezwa kesho Jumatano katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.





