Mzungu wa Singida avunja mkataba
Sisti Herman
November 3, 2026
Share :

Siku moja baada ya Mohamed Damaro kuvunja mkataba wake na Singida Black Stars, nyota mwingine wa timu hiyo, Marcelo Canadi naye amefuata nyayo zake.
Mshambuliaji huyo raia wa Austria, ametangaza rasmi uamuzi huo leo Jumanne, Novemba 3, 2026.
Canadi amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kufanya mazungumzona klabu hiyo aliyoitumikia kwa miezi minne tu.
"Wakati mwingine katika mpira wa miguu, mambo huwa hayaendi kama tunavyotegemea. Baada ya mazungumzo na klabu, nimeamua kwamba muda wangu hapa umefikia mwisho.
"Asante Tanzania kwa kuwa na mimi. Tutaonana tena siku moja," amesema Canadi.
Canadi anaondoka akiwa ameifungia Singida Black Stars bao moja kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo alilipata katika mechi dhidi ya Namungo FC ambayo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.





