Nabi uso kwa uso na Gamondi, Kaizer Chiefs vs Yanga sc
Joyce Shedrack
July 8, 2024
Share :
Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Yanga SC watashiriki mashindano ya Toyota Cup yanayoandaliwa na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini itakayofanyika kwenye Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein tarehe 28 Julai, 2024.
Yanga watatumia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi ya msimu mpya (Pre Season).
Klabu ya Kaizer Chiefs kwa sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga Nasriddine Nabi aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea As Far Rabat ya Morocco.