Nabii Emmanuel apigwa marufuku kuingia Casino kwasababu ya kushinda sana
Eric Buyanza
June 8, 2024
Share :
Nabii wa Zimbabwe Emmanuel Mutumwa, aliyedai Mungu amempa formula ya kushinda kwenye majumba ya kamari (Casino) amepigwa marufuku kuingia kwenye makasino mengine baada ya hivi juzi kushinda $30,000 (Milioni 80) kwenye casino ndogo ya mtaani ikiwa ni mfululizo wa ushindi ambao amekuwa akiupata mara kwa mara.
Akizungumzia kufungiwa kwake, Nabii Emmanuel Mutumwa, alisema;
"Huu ndio ushindi mkubwa zaidi kuwahi kurekodiwa kwenye kasino ndogo...nimevunja rekodi yangu ya awali kwa karibia mara mbili, hata hivyo furaha yangu imekatishwa baada ya kupigwa marufuku kuingia kwenye Casino zingine kwasababu ya kushinda mara nyingi.... wanaogopa watafilisika”
Nabii Emmanuel anasema amekuwa akitumia pesa hizo kulipa karo ya shule kwa baadhi ya watoto wa waumini wa kanisa lake na pia kutoa mtaji wa biashara kwa waumini wake.
Msimamizi wa moja ya kasino ndogo za mtaani mjini Bulawayo alithibitisha kuwa kampuni za kamari kwa kawaida huzuia au kufunga akaunti za wale wanaoshinda mara kwa mara, na sera hiyo inalenga kulinda utulivu wa kifedha wa Casino hizo.