pmbet

Nadhani kwa sasa Arsenal ndio timu bora zaidi Ulaya - Régis Le Bris

Eric Buyanza

September 12, 2026
Share :

Kocha mkuu wa klabu ya Sunderland, Régis Le Bris, ametoa sifa kubwa kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza, Arsenal FC, akitangaza kuwa ndiyo timu inayocheza soka safi na bora zaidi barani Ulaya kwa wakati huu.

 

Kauli hiyo ya Le Bris inakuja wakati kikosi chake kikijiandaa kwa mtihani mzito wa kuwakaribisha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza (Arsenal) katika dimba la Stadium of Light.

 

Akizungumza kwa unyenyekevu na waandishi wa habari kuelekea mtanange huo, Le Bris alikiri kuvutiwa mno na jinsi kocha Mikel Arteta alivyosuka kikosi chake.

"Ingawa bado ni mapema kwenye msimu, wanaonekana kuwa imara kila mahali, kuanzia kwenye benchi lao na kila idara, nadhani kwa sasa wao ndio timu bora zaidi Ulaya. Wana kasi na morali kubwa sana" alisema Le Bris.

 

Licha ya kuwapa sifa hizo kubwa, Le Bris amewataka wachezaji wake kutokuwa waoga na badala yake wacheze kwa kujiamini na kulinda utambulisho wa soka la Sunderland. Alibainisha kuwa mbinu ya kujihami kupita kiasi huwa haisaidii wanapokutana na timu kubwa. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet