"Nafanya muziki kujifurahisha, na sio kazi" - Young Killer
Eric Buyanza
March 26, 2024
Share :
Rapa Young Killer amesema anafanya muziki kujifurahisha na siyo kazi anayoitegemea kuendesha maisha, na hicho ndicho kinacho mtofautisha yeye na wanamuziki wengi wa Tanzania.
“Kazi ya muziki kwangu ni kufurahi na marafiki na mashabiki zangu na sitoi macho kama kazi inayoendesha maisha yangu, ndio maana ngoma zangu zinapishana muda mrefu tofauti na ilivyo kwa wasanii wengine ambao hutoa ngoma hapa kwa hapa,” amesema Young Killer.
Msanii huyo amesema anajivunia umaarufu aliokuwa nao ambao umetokana na muziki huo lakini siri ya jina lake kuwa kubwa ni kufanya muziki wa peke yake usiofanana na rapa yeyote nchini.
TSN