Nafanya rotation kwasababu maalum - Gamondi
Sisti Herman
December 17, 2023
Share :
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amewajia juu mashabiki na wadau wanaohoji kuhusu uhitaji wa mabadiliko ya mara kwa mara ya kikosi ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengi zaidi kupata nafasi ya kucheza huku akitoa sababu maalum zinazoweza kumlazimu kufanya “rotation” ya kikosi na sio kwa kushinikizwa na mashabiki
“Nina wachezaji wawili walioadhibiwa, wachezaji wawili majeruhi halafu ndani ya siku 15 tunacheza mechi 5, hizi ndiyo sababu za kufanya mabadiliko ya wachezaji na si zingine” alisema Gamondi kwenye mahijiano na PMTV
Gamondi ameyasema hayo jana kwenye mahojiano baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar, Yanga ikishinda goli 4-1
Fuatilia mahojiano haya kwenye mtandao wa Youtube wa PMTV