pmbet

Nahodha wa MV Mwanza asimamishwa kazi

Sisti Herman

November 26, 2026
Share :

 

Nahodha aliyekuwa akiendesha meli ya New MV Mwanza ilipopata ajali ya kugonga mwamba ndani ya Ziwa Victoria jijini Mwanza, amesimamishwa kazi baada ya uchunguzi wa kitaalamu kubaini kuwa tukio hilo lilisababishwa na makosa ya kibinadamu (Human Error), badala ya hitilafu za kiufundi.

Akizungumza leo Novemba 26, 2026 na waandishi wa habari, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema uchunguzi umebaini kuwa ajali hiyo ilichangiwa na upungufu wa uzoefu na umahiri katika uendeshaji wa mifumo ya kisasa ya meli hiyo.

Amesema injini na mifumo muhimu ya meli hiyo iko salama na haikuathiriwa, huku akibainisha kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa na hakuna uchafuzi wa mazingira uliotokea.

Profesa Mbarawa ameliagiza Shirika la Meli nchini (Tashico) kumsimamisha kazi nahodha huyo, kufanya matengenezo ya sehemu ya mbele ya meli iliyoharibika na kuchukua hatua stahiki kwa watumishi wengine watakaobainika kutotekeleza wajibu wao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet