Nahodha wa SC Villa ya Uganda afariki Dunia.
Joyce Shedrack
August 5, 2026
Share :
Nahodha wa klabu ya SC Villa, David Owori, amefariki dunia baada ya kuripotiwa kushambuliwa na majambazi alipokuwa akirejea nyumbani usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Owori alipata majeraha mabaya katika shambulio hilo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu, lakini baadaye alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.
Nahodha huyo wa SC Villa mwenye umri wa miaka 27 alijumuishwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) kilichojiandaa na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zilizofanyika nchini Morocco Disemba mwaka jana.
Uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea huku mamlaka zikisaka waliohusika na shambulio hilo.





