Nahodha wa Timu ya Taifa ya Liberia afariki dunia
Sisti Herman
November 27, 2026
Share :

Aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Liberia 🇱🇷, Allen Njie (27), anaripotiwa kufariki dunia nchini Marekani baada ya kuanguka ghafla akiwa katika hafla fulani.
Mchezaji huyo wa zamani aliyekuwa akicheza eneo la kiungo alikimbizwa kupata matibabu, lakini baadaye ilithibitishwa kuwa amefariki dunia.
Alistaafu soka la kulipwa takriban miaka minne iliyopita kutokana na tatizo la moyo.
Taarifa zaidi kuhusu mazingira ya kifo chake bado hazijawekwa wazi.





