Najim chini ya Management ya Zimbwe na Kibu, Carl Pro Int.
Sisti Herman
May 16, 2024
Share :
Kampuni ya usimamizi wa michezo ya Carls Pro International Limited imethibitisha kumuongeza kwenye familia yako kiungo mshambuliaji wa Tabora United, Najim Mussa ambaye amekuwa na kiwango bora tangu kupanda daraja na klabu hiyo.
Najim amejiunga na kmapuni hiyo ambayo pia inawasiamamia Mohammed Hussein Zimbwe, Kibu Denis,Mzamiru Yassin wa Simba pamoja na Bakari Mwamnyeto na Zawadi Mauya wa Yanga.
Ikumbukwe mchezaji huyo alifunga goli la pekee la Tabora United ambalo lilikuwa halali dhidi ya Simba kabla halijakataliwa na mwamuzi.