"Najivunia kupita mikono ya Morinyo" - Clara
Sisti Herman
February 19, 2024
Share :
Mchezaji wa klabu ya Al Nassr ya wanawake, Mtanzania Clara Luvanga amebainisha kuwa anajivunia kuwa mmoja wa wachezaji waliopita kwenye mikono ya kocha maarufu zaidi mwanamke Tanzania Edna Lema “Mourinho” ambaye walikuwa na nyakati bora siku zilizpotita.
“Edna Lema kocha wa mpira kila mcezaji aliyepita kwenye mikono yako atalitaja jina lako, najivunia kupita katika mikono yako mpaka hapa nilipofika” - aliandika Clara kupitia mitandao yake ya kijamii
Clara na Edna walikuwa wote Yanga Princess misimu kadhaa iliyopita huku pia Edna akiwa kocha wa timu za Taifa za wanawake.