Najuta kwa kutompa Joe Hart nafasi - Pep Guardiola
Eric Buyanza
May 23, 2026
Share :

Kocha anayeondoka wa Manchester City, Pep Guardiola, amekiri kuwa anajutia kutompa nafasi Joe Hart baada ya kuwasili katika klabu hiyo mwaka 2016.
Hart hakucheza mchezo hata mmoja chini ya Guardiola na alicheza kwa mkopo Torino kwa misimu miwili na baadae kujiunga na Burnley.
Kipindi hicho mlinda mlango huyo alikuwa kipa namba moja wa timu ya taifa ya Uingereza.
Lakini Guardiola aliona Hart hakuwa mzuri na akamleta Claudio Bravo.
"Nataka kukiri kitu, nina kitu kimoja najuta sana - sikumpa Joe Hart nafasi ya kuthibitisha jinsi alivyo golikipa bora.......unapofanya maamuzi mengi wakati mwingine unafanya makosa" alisema Guardiola alipokuwa akiongea na Sky Sports.





