pmbet

Namshukuru mke wangu, alinifanya nikaacha madawa - Mr Blue

Eric Buyanza

March 8, 2024
Share :

Kila binadamu aliyefanikiwa katika jambo fulani, basi hakika lazima atakuwa na hadithi ya safari yake.
 

Tunasema hivyo kwasababu msanii Mr Blue 'Byser' ni mmoja ya watu wenye hadithi yenye kuvutia kwenye safari ya maisha yake, ikumbukwe msanii huyu alianza muziki na kupata mafanikio akiwa mdogo sana.
 

Kwenye mahojiano ya hivi karibuni na BBC, msanii huyo ambaye jina halisi ni Khery Sameer Rajab, amemtaja mke wake kuwa ndiye aliyemsaidia kuachana na utumiaji wa madawa ya kulevya.
 

Kwa mujibu wa Mr Blue,... marafiki na watu waliomzungunguka kipindi hicho akiwa 'Hot' ndio waliompotosha akajikuta anajiingiza kwenye makundi mabaya yaliyopelekea utumiaji mkubwa wa pombe na madawa ya kulevya.
 

"Mke wangu namshukuru sana kwani yeye ndiye amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kubadilika, alikuwa ananiambia taratibu vitu vya kufanya na baadae aliposhika ujauzito ndio nikagundua naenda kuwa na familia"
 

"Mimi wakati naanza muziki nilikuwa mtoto na sikuwa na rafiki, lakini watu walikuja wakijifanya wananijua wamesoma na mimi kwahiyo ule ushikaji mtu akichoma na mimi nachoma mara pombe......nikawa siendi studio,  niliharibiwa na watu waliokuja baada ya mimi kuwa maarufu... namshukuru Mungu na mke wangu nimerudi kwenye mstari” anasema Mr Blue.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet