pmbet

Namungo FC waitumia barua ya wazi Simba

Eric Buyanza

October 31, 2026
Share :

Siku mbili kabla ya pambano la Simba na Namungo FC, kikosi cha Namungo FC kimeiandikia barua Simba ya kwamba wamesikitishwa na taarifa za malalamiko kutoka timu ndogo ndogo zilizofungwa  na Simba kabla ya kukutana na wao.

 

Barua hiyo iliyochapishwa katika ukurasa rasmi wa Namungo FC ina kichwa cha habari kisomekacho KUTETEA WANYONGE.

 

“ YAH : KUTETEA WANYONGE


Rejea kichwa cha habari hapo juu, Namungo Fc tumeskikitishwa sana na taarifa za malalamiko kutoka timu ndogo ndogo mlizozifunga kabla ya kukutana na sisi.

 

“ Wauaji wa kusini tumelibeba swala hili na kuwa jambo la kitaifa,hivyo tutahakikisha tunawapiga kipigo cha paka mwizi ili iwe fundisho.

 

“ Tunapenda kuwakumbusha kuwa hakuna njia ya kukwepa kipigo hiki hata kuwe na Elininyo.

WAKO MUUAJI WA KUSINI
Namungo Football Club” iliandikwa taarifa ya Namungo FC.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet