Namungo waachana na Kitambi, Ihefu na Geita wahusishwa naye
Sisti Herman
December 14, 2023
Share :
Uongozi wa Namungo siku ya jana ulitangaza kuachana rasmi na kocha wao mkuu Denis Kitambi.
Kocha huyo anakuwa wa pili msimu huu kuondoka kikosini hapo baada ya Cedric Kaze ambaye alijiuzulu Oktoba 22.
"Uongozi wa Namungo FC unapenda kumshukuru Kocha Denis Kitambi kwa muda wote aliotumikia timu kwa ushirikiano mkubwa ndani ya timu yetu," imeeleza taarifa ya Namungo.
Duru mbalimbali za habari zinamhusisha kocha huyo kujiunga na timu za Geita Gold na Ihefu FC.