Nani kutwaa ubingwa Afcon leo? Ivory Coast au Nigeria
Sisti Herman
February 11, 2024
Share :
Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) inatarajiwa kufanyika katika dimba la Alassane Ouattara jijin Abidjan, ambapo Timu za Nigeria, The Super Eagles na wenyeji Ivory Coast zitakutana katika kuwania Ubingwa.
Mtanange huo utapigwa leo Jumapili ya Februari 11, 2024 Saa 5 usiku na kushuhudiwa na mashabiki takriban 60,000 watakaokuwa Uwanjani pamoja na Mamilioni wengine watakaoutazama Duniani.