Naona aibu kuona watoto wanazuiwa wasiende shule - Biteko
Eric Buyanza
June 8, 2024
Share :
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu kwa kuwa ndio nguzo ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Dkt.Biteko amesema serikali imeendelea kujenga shule ambapo kwa sasa Wilaya ya Bukombe ina shule za sekondari 7 na shule 5 za kidato cha tano na sita ambapo awali kulikuwa na shule moja.
"Naona aibu kuona watoto wanazuiwa wasiende shule, niwaombe wazazi tupeleke watoto shule. Wenyeviti wa Vijiji niwaombe kama kuna mtoto kwenye kijiji chako ambaye anatakiwa kwenda shule na haendi, nenda kwenye kaya hiyo kuwaeleza kuhusu umuhimu wa elimu ili mtoto huyo aweze kwenda shule" Amesema Dkt. Biteko.
Biteko amechangia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya shule iliyopo katika Kata ya Bugelenga kwa kutoa mabati 135 na mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali.