pmbet

"Naondoka Barcelona" - Xavi

Sisti Herman

January 28, 2024
Share :

Baada ya klabu Barcelona kukubali “kichapo cha mbwa mwizi” cha magoli 5-3 kutoka ‘nyambizi wa manjano’ Villarreal kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Hispania (La Liga) katika dimba la nyumbani la Olímpic Lluís Companys, Barcelona, kocha wa timu hiyo Xavi Hernandez amesema wazi kuwa ifikapo mwishoni mwa msimu huu anawajibika kuondoka.

 

“Nimefikia ukomo, ni wakati wa mabadiliko, nadhani ni wakati wangu wa kuondoka, nimeongea na bodi na nitaondoka june 30” alisema Xavi kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya mchezo.

Kwenye mchezo huo uliomalizika kwa matokeo hayo mabaya kwa Barca,magoli ya Barcelona yalifungwa na  Gundogan 60’, Pedri 68’ huku beki wa Villareal akijifunga Bailly (og) 71’ na magoli ya Villareal yalifungwa na Moreno 41’, Akhomach 54’, Guedes 84’, Sorloth 90+9’  na Morales 90+11’

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet