pmbet

"Naondoka Liverpool" - Klopp

Sisti Herman

January 26, 2024
Share :

Kocha mkuu wa Liverpool ametoa taarifa kwa mashabiki, wanachama, viongozi wa klabu ya Liverpool kuwa hatoendelea kuwa kocha wa timu hiyo baada ya msimu huu wa 2023/23 kutamatika.

 

Taarifa ya Klopp kwa umma

 

"Ninaweza kuelewa kuwa ni mshtuko kwa watu wengi wakati huu na unapoisikia kwa mara ya kwanza, lakini ni wazi naweza kuelezea - ​​au angalau kujaribu kuelezea".

 

"Ninapenda kila kitu kuhusu klabu hii, jiji, wafuasi wetu, timu, wafanyakazi. Napenda kila kitu”.

 

“Nimekwisha uambia uongozi tangu mwezi wa 11 kuwa, Mimi naondoka”.

 

"Tulipokaa pamoja na klabu tukizungumza kuhusu wachezaji wanaoweza kusajiliwa, kambi ya majira ya joto ijayo na tunaweza kwenda popote… wazo lilikuja na lilikuwa jipya!".

 

"Nilihisi kama sina uhakika kama ntaendelea kuwepo hapa”.

 

"Nilishangaa na kuanza kufikiria juu yake, sasa uamuzi umethibitishwa: Ninaondoka".

 

"Baada ya miaka ambayo tulikuwa pamoja na baada ya muda wote tulioishi pamoja na pia baada ya mambo yote tuliyopitia pamoja, heshima ilikua kwenu, upendo uliongezeka kwenu na deni langu kubwa kwenu ni kweli".

 

"Kwangu ilikuwa muhimu sana kwamba ninaweza kusaidia kurudisha timu hii kwenye reli ... na ilikuwa tu nilitaka".

“Hebu tushinde kila kitu katika msimu huu”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet