Nashutumiwa kutumia uchawi, kisa sinyoi makwapa - Burna Boy
Eric Buyanza
August 23, 2025
Share :
Kutoka nchini Nigeria mwanamuziki Burna Boy, amezungumzia dhana potofu inayoenezwa juu yake ya kwamba hapendi kunyoa nywele za makwapa kwa sababu ndicho chanzo cha mafanikio yake, wakimaanisha anazitumia kama uchawi wa kupatia pesa na umaarufu.
Itakumbukwa picha kadhaa ambazo amewahi kupigwa msanii huyu zimekuwa zikiyaonesha makwapa yake yakiwa hayajanyolewa.
Kwenye mahojiano ya hivi majuzi na Apple Music, nyota huyo alielezea madai hayo kuwa ya kufurahisha.
SWALI: Ni dhana gani potofu inayozungumzwa kuhusu Burna Boy?
BURNA BOY: Kuna baadhi ya watu wanaodai kwamba kwapa langu ndipo nguvu zangu ziko kwa sababu sinyoi.