Nataka kila mchezaji wa Simba afunge - Fadlu
Eric Buyanza
December 3, 2024
Share :
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amesema anatengeneza mfumo ambao utawawezesha wachezaji wake wote kuweza kufunga mabao au kutoa pasi za mwisho kwa manufaa ya timu na si kutegemea mastraika pekee kufunga.
"Natengeneza kikosi ambacho kitakuwa na ushirikiano, kitacheza kama timu, mafanikio hayawezi kumtegemea mchezaji mmoja ndiyo afunge mabao, kila mmoja anatakiwa achangie ushindi, ni golikipa tu ndiyo kazi yake itakuwa ni kuzuia mabao yasiingie wavuni waliobaki wote pamoja na majukumu yao mengine, lakini wanatakiwa wachangie 'asisti' na kufunga mabao pia," alisema kocha huyo.
👉NIPASHE