pmbet

"Nataka kuzaa watoto wa kiume zaidi" – Tiwa Savage

Eric Buyanza

September 17, 2025
Share :

Kutoka nchini Nigeria mwanamama mkali wa miondoko ya Afrobeats, Tiwa Savage, amefunguka kuhusu maisha yake ya binafsi huku akiweka wazi nia ya kupanua familia yake. 

Katika mahojiano ya hivi karibuni mwanamama huyo alisema anaona kabisa akienda kupata watoto zaidi. 

Tiwa ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja wa kiume aitwae Jamil Balogun mwenye umri wa miaka 10, amefichua hamu yake kubwa ya kuongeza idadi ya watoto wa kiume.

"Nataka watoto zaidi, wa kiume. Ninajiandaa tu. Kama nilivyosema, mimi si mdogo. Ninafikiria kuhusu umri wangu na nataka kutumia mayai yangu yakiwa bado na afya," alisema.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet